Picha 9:Kinondoni yatinga visiwani Zanzibar baada ya kuondoka Simba, Yanga na Prison

0

Zanzibar ilikua na ugeni wa timu 3 za ligi kuu Tanzania bara amabazo zilifunga kambi hapa visiwani. ikiwa Simba pamoja na Tanzania Prison ziliweka kambi hapa unguja na Yanga kuweka kambi huko kisiwani Pemba. Baada ya kuondoka kwa timu hizo za ligi kuu bara tayari tumepokea ugeni mwengine kutoka Tanzania bara mara hii ni timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza bara timu ya Kinondoni KMC ilioweka kambi hapa visiwani Zanzibar.

Zsports tuliweza kuitembelea timu hiyo inayofanya mazoezi katika viwanja vya mnazi mmoja na tuliweza kuongea na kocha mkuu wa timu hiyo Fred Filix Minziro na amesema wamechagua kuja visiwani Zanzibar kwasababu ya utulivu pamoja na kupata mechi za kirafiki. Timu hiyo itakuepo hapa kwa takribani wiki 3

Na: Said Salim (Press Hazard)

LEAVE A REPLY