Picha: Kevin Hart na Ray J wafunga ndoa na wachumba wao

0

Mastaa wa Marekani, Kevin Hart na Ray J, wamefunga ndoa na wachumba wao mwishoni mwa wiki.

Hart ambaye ni mchekeshaji na muigizaji wa filamu, amefunga ndoa Jumamosi na mpenzi wake wa muda mrefu, Eniko Parrish huko California.

13774739_1049819128442723_1772704471_n

Wote wameshare picha za ndoa yao kwenye Instagram. Mtoto wake wa kiume, Hendrix ndiye alikuwa best man wake.

Kwenye moja ya picha alizoweka, Kevin ameandika: kevinhart4realMr & Mrs HART!!!!! In Love & Loving it!!!! #Married #DopePic.”

13671240_319461665061900_1245212590_n

Kwa upande wake Eniko ameandika: Some people wait a lifetime for a moment like this… ? #MrsHart???? #VeraWangGang.”

Naye muimbaji wa RnB, Ray alifunga ndoa na mpenzi wake Princess Love Ijumaa huko Vibiana, Los Angeles.

princess-love-ray-j

The Game alikuwa miongoni mwa wanaume nane waliomsindikiza Ray J huku dada yake, Brandy akiwa msindikizaji wa bibi harusi.

13573436_1671622249826809_1097808815_n

Kulikuwepo na wageni takriban 150.

LEAVE A REPLY