Bonta na Lord Eyez walishindwa kuisoma kasi ya Weusi !

0

Kutofautiana katika Kundi huwa kunapelekea kutengana na wakati mwingine Kuvunja mahusiano  na kusababisha matabaka ambayo yanaweza kusitisha malengo au madhumuni ya muungano wa kundi.

Weusi ni miongoni mwa makundi bora zaidi na yenye nguvu hasa katika muziki wa Hip-hop hapa nchini,lakini Weusi tayari inamatabaka ndani yake kitu ambacho kimekuwa hakijawahi kupatiwa jibu sahihi kwa kila mmoja wao katika kundi pindi anapokua amekuwa akikutana na swali linalo gusia juu ya  umoja wao kama kundi katka kazi.

Weusi inajumla ya Wasanii watano ambao ni Joh makini,Gnako,Nkki wa pilli,Bonta,pamoja na Lord eyez kama ilivyo tambulisha kwa mara ya kwanza na kazi yao kama kundi  iliyowatambulisha ilikua inaitwa Nyota ya watoto wa Mungu nyimbo ambayo wasanii wote watano walisikika katika kazi hiyo  na kuashilia kuwa mwendo utakuwa ni huo huo wa kusikika wasanii wote katika kazi ya kundi.

Kwakuwa kabla ya kutengenezwa kwa Weusi kila msanii wa kundi la Weusi alikua ananafasi yake katika muziki huu  kutokaka na uwezo wake binafsi hali ambayo haikuwa na hofu kubwa juu yao na hata kwa mashabiki wao ambao nao walikusanyika na kuwa kitu kimoja kutokana na kuwepo kwa kundi la Weusi.

Kazi nyingi zimepita zikiwa zinatambulika kama za kundi la Weusi lakini cha kushangaza baadhi ya wasanii wanao unda kundi hilo wamekuwa hawasikiki katika kazi hizo hasa hasa kwa Lord eyez na Bonta,hali ambayo imekuwa ikizuwa maswali mengi sana  japo wao kama Weusi kwa umoja wao Wanajua misingi na taratibu ambazo wamejiwekea kiasi kwamba wangekuwa wameiweka wazi hata kwa mashabiki wao huenda ingewafanya wajue sababu hasa inayopelekea kuwepo na tabaka miongoni mwao hasa katika kazi na kuondoa adha ya maswali ambayo yamekuwa yakijirudia kila wakati.

Weusi ya mtu tatu yakwao Nikki wa Pilli,G Nako na Joh Makini  imekuwa ikibadilika badilika sana katika kazi wanazo zitoa, zimekuwa na usasa mwingi na kuewndana na mambo ambayo yanakuwa yananafasi kubwa sana katika jamii hiyo ni kutokana na kujikita zaidi katika muziki wa biashara na hata ukaribu wao wa Weusi ya mtu tatu umekuwa ni mkubwa kuliko ukaribu wa Weusi ya mtu tano.

Lord Eyez na Bonta, wameonekana wakiwa nyuma sana na kasi ya ufanyaji kiazi ya weusi ya mtu tatu kiasi cha kufikia hatua ya wao kufanya kazi ambazo zimekuwa hazina mabadiliko makubwa ukilinganisha na kazi ambazo wamekuwa wakizitoa Weusi ya mtu tatu hata katika kazi zao binafsi za nje ya kundi.

Kutokubadilika kwa Lord Eyez na Bonta kunapelekea kusiwape nafasi yakutoa mchango wao katika kazi na kunakila dalili za kushtukia kazi ya kundi imesha toka bila wao kujua ilirekodiwa lini na ilipitishwa vip kwenda kwa mashabiki wao.

Ukisikiliza kwa umakini kazi za Bonta na ‘Lord Eyez’ utagundua kuwa hakuna mabadiliko ya ‘style’ ya uimbaji wala uandishi zaidi ya kuona mabadiliko ya katika uandaaji tu wa studio ambazo wamekuwa wakifanyia kazi zao.

Hivyo basi ni wazi kabisa na hatuna budi kukubali kuwa Lord eyez na Bonta wameshindwa kuendana na kasi ya weusi na ndio mana imekuwa ni ngumu sana kuwasikia katika kazi za pamoja kutokana na Weusi ya mtu tatu tayari imejitengenezea ‘Chemistry’ ambayo inanguvu kubwa kati yao watatu.

KUWA NASI NIPOLIVE.COM

Usisite Kuwa nasi katika FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote mpya! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kutoka Nipolive.com!

LEAVE A REPLY