Serikali kuja na mfuko wa bima kwa jeshi la ulinzi

0

Na Jasmine Shamwepu,Dodoma.

SERIKALI imesema ipo kwenye mchakato wa kuanzisha mfuko wa Bima ya Afya kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni mjini Dodoma na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa dokta HUSSEIN MWINYI wakati akijibu swali la mbunge wa Welezo SAADA MKUYA.

Katika swali lake mbunge huyo amehoji mikakati madhubuti ambayo serikali imeweka wa kuhakikisha kuwa vifaa tiba,dawa na madaktari wanapatikana ili kutoa huduma bora.

Dokta MWINYI akijibu swali hilo amesema ni  imani ya serikali kuwa mfuko huo utakapoanzishwa utaweza kuongeza rasilimali fedha katika utoaji huduma za afya jeshini.

Amesema fedha za ziada zitatumika katika kuboresha miundombinu na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na hivyo kuboresha huduma za afya kwa wanajeshi na wananchi wanaotumia vituo vya afya  vya jeshi kupata tiba.

Ameeleza kuwa wizara  inaendelea na hatua ya kuboresha huduma za tiba jeshini kwa kuendeleza kushawishi wataalam wa tiba wenye sifa kujiunga na jeshi hilo kulingana na nafasi za ajira.

KUWA NASI NIPOLIVE.COM

Usisite Kuwa nasi katika FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote mpya! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kutoka Nipolive.com!

LEAVE A REPLY