Jux: Wajue kwanza mashabiki wa muziki wangu

0

Msanii wa R&B Nchini  Juma Jux awataja wanawake kuwa ndio mashabiki wa muziki wake kwa kiasi kikubwa tofauti na mashabiki wake wa kiume.

Mkali huyo wa ‘Uzuri Wako’ ameamua kueleza kuwa mashabiki wa muziki wake walio wengi wanawake na ndio wanao onesha upendo mkubwa hata wakiwa katika maonesho mbali mbali na kusema wanawake wamekuwa wakiguswa sana tofauti na wanaume ambao hawaoneshi upendo dhahili kama ilivyo kwa wanawake.

‘’Mashabiki wa muziki wa Jux ni wanawake na ninasema hivyo kwa sanbabu ndio wamekuwa wakionesha hisia zao kwa kiwango kikubwa tofauti na wanawake hasa pale napokuwa jukwaani  na hilo ndio linanipa sababu za kujua kuwa wapenzi wa muziki wangu ni wanawake ‘’ amesema Jux.

Hata hivyo, jux ameongeza kuwa mara nyingi anapokuwa jukwaani anapenda kuvua shati na kubaki kifua wazi na hiyo yote ni kwaajiri ya mashabiki wake hasa wanawake.

Jux  ametengeneza historia kwa mara ya kwanza katika muziki wake kwa kupata watazamaji zaidi ya milioni moja kwenye video ya Utaniua ndani ya wiki tatu na kutengeneza historia ambayo haijawahi kufikiwa na nyimbo zake zingine ambazo amekwisha zitoa hapo mwanzo.

KUWA NASI NIPOLIVE.COM

Usisite Kuwa nasi katika FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote mpya! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kutoka Nipolive.com!

 

LEAVE A REPLY