Harry Kane aibeba Spurs ugenini na kuweka rekodi

0

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur, Harry Kane jana usiku ametupia magoli matatu dhidi APOEL Nicosia na kuweka rekodi msimu huu kuwa mchezaji wa kwanza kupiga Hatrick kwenye michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya.

Kane alianza kufungua akaunti ya magoli kunako dakika ya 39 kipindi cha kwanza na kutupia magoli mawili kipindi cha pili huku APOEL ikishindwa kufurukuta nyumbani kwake.

Kwenye msimamo Spurs wapo nafasi ya pili katika kundi H linaloongozwa na Real Madrid wote wakiwa na pointi 6 wakipishana kwenye tofauti ya magoli.

LEAVE A REPLY