Batuli:kila mtu atakuwa na hamu mimi

0
STAA wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amesema kuwa, anafurahi  alivyokaa kimya kwa maana kufanya hivyo kunawafanya mashabiki wake wasimchoke na  kummisi.
Batuli aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, anaamini kabisa siku akiibuka na kitu chake  chochote, kila mtu atakuwa na hamu nacho kwa sababu hawajamuona kwa muda mrefu.
“Mimi nafurahia sana watu kusema nimepotea hivi kwa sababu siyo kila wakati watu wajue mambo yako, wakuseme hovyohovyo, lakini ukiwa kimya kwa muda mrefu, ukiibuka, kila mmoja atakuwa na hamu na wewe,” alisema Batuli.

LEAVE A REPLY