BALA LA NJAA LA NUKIA KWA WAKAZI WA KIHESA KILOLO

0

Kufuatia uwepo wa zuio la serikali la kuwataka wananchi wa Kihesa kilolo Manispaa ya Iringa kutojihusisha na shughili zozote hususani kilimo katika eneo lililotengwa kwaajili ya kuendeleza kupitia sekta ya utalii wananchi hao wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo kuwaruhusu watumie eneo hilo katika kipindi cha mwaka mmoja ndipo watafute eneo jingine kwa shughuli zao.

Eneo la kihesa kilolo ni miongoni mwa maeneo yaliyopo katikati ya mji wa Iringa ambapo awali lilikuwa likitumiwa na wananchi hao kama eneo la uzarishaji wa chakula huku likiwasaidia kujipatia mahitaji mengine kupitia eneo hilo jambo linalozua sintofahamu kwa wananchi hao kwa kukosa eneo kwaajili ya kilimo huku wakikabiliwa na hofu ya kukumbwa na njaa.

Miongoni mwa wananchi wa eneo hilo wakizungumza Mbele ya mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela katika mkutano wake uliolenga kutoa ufafanuzi juu ya zuio hilo wanasema iwapo serikali haitawaruhusu kutumia eneo hilo wapo hatarini kukumbwa na njaa kwani hakuna maandalizi yoyote ya kutafuta eneo jingine hivyo wameiomba serikali kuwaongezea muda kulitumia eneo hilo.

Akijibu maombi hayo mkuu huyo wa wilaya ya Iringa amesema kutokana na Agizo hilo kutolewa na Waziri mwenye Dhamana ya Maliasili na Utalii kwa nafasi yake hana mamlaka ya kutengua agizo hilo badala yake ni kuwahamasisha wananchi kutafuta maeneo mengine kwaajili ya kilimo na si vinginevyo.

LEAVE A REPLY