Watakaoshindania Tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika kutangazwa 2017

0

Wachezaji watano ambao watashindania Tuzo ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa BBC mwaka 2017 watatangazwa baadaye leo Jumamosi, 11 Novemba.

Majina hayo yatatangazwa wakati wa kipindi maalum cha moja kwa moja katika BBC World News, BBC World Service na BBC Sport Online kuanzia saa 18:00 GMT (saa tatu usiku Afrika Mashariki).

Waliowahi kushinda tuzo hiyo awali ni pamoja na nyota wawili wa Ivory Coast Didier Drogba na Yaya Toure, Jay-Jay Okocha wa Nigeria na jagina wa Liberia George Weah.

Jopo ambalo litawashirikisha miongoni mwa wengine Emmanuel Amuneke, mshindi wa ubingwa Afrika na Olimpiki 1996, Arnaud Djoum, mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 akiwa na Cameroon, na Jean Sseninde, kutoka Uganda anayechezea Crystal Palace Ladies, watakuwepo kujadili majina ya wataoteuliwa kushindania tuzo hiyo.

Watano hao watakuwa wakitumai kufuata nyayo za mshindi wa mwaka jana Riyad Mahrez, aliyeng’aa mwaka 2016 akichezea mabingwa wa Ligi ya Premia mwaka huo Leicester City na Algeria.

Mshindi wa tuzo ya mwaka jana, Mahrez alisema: “Ina maana kubwa sana kwangu; ni jambo kubwa na muhimu kwa wachezaji wa Afrika na hivyo basi nina furaha sana, najionea fahari. Kwa wachezaji wa Afrika, ni heshima kubwa.”

Peter Okwoche na Mimi Fawaz watatangaza kipindi hicho maalum cha Ijumaa mbele ya haadhira ukumbini London, mashabiki nao wakifuatilia pia mitandao ya kijamii.

Mashabiki wanaweza kupigia mchezaji wanayetaka ashinde kupitia ukurasa wa soka ya Afrika katika tovuti ya BBC, BBC African football, kuanzia saa 19:00 GMT Jumamosi, 11 Novemba hadi upigaji kura utakapokamilika 18:00 GMT Jumatatu, 27 Novemba.

Mshindi atatangazwa moja kwa moja 17:30 GMT Jumatatu, 11 Desemba.

Washindi wa zamani wa tuzo ya mchezaji bora ya BBC :

2016 – Riyad Mahrez (Algeria na Leicester City)

2015 – Yaya Toure (Ivory Coast na Manchester City)

2014 – Yacine Brahimi – Algeria na FC Porto (Ureno)

2013 – Yaya Toure (Ivory Coast na Manchester City)

2012 – Chris Katongo (Zambia na Chinese Construction)

2011 – Andre ‘Dede’ Ayew (Marseille na Ghana)

2010 – Asamoah Gyan (Sunderland na Ghana)

2009 – Didier Drogba (Chelsea na Ivory Coast)

2008 – Mohamed Aboutrika (Al Ahly na Misri)

2007 – Emmanuel Adebayor (Arsenal naTogo)

2006 – Michael Essien (Chelsea Na Ghana)

2005 – Mohamed Barakat (Al Ahly Na Misri)

2004 – Jay Jay Okocha (Bolton na Nigeria)

2003 – Jay Jay Okocha (Bolton na Nigeria)

2002 – El Hadji Diouf (Liverpool na Senegal)

2001 – Sammy Kuffour (Bayern Munich na Ghana)

2000 – Patrick Mboma (Parma na Cameroon)

LEAVE A REPLY